
NURU YA UPENDO
June 10, 2025 at 04:02 PM
*MAOMBI YA USIKU.*
JUMANNE[10.06.2025].
JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO LIBARIKIWE SANA.
KARIBU KATIKA MAOMBI YA USIKU VIPENGELE VITATUMWA KILA SIKU USIKU UNAOMBA WAKATI WA KULALA UKISHAMALIZA KULA CHAKULA CHAKO SIO MAOMBI YA MFUNGO.
*NENO KUU*: *KWA NEEMA TUNAOKOLEWA.*
Marko 8:22-26
"Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? -Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda.Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie."
.✓ *VIPENGELE VYA MAOMBI YA LEO JUMANNE.TUNAOMBA* *KWA AJILI YA NEEMA TELE.*
✓Mshukuru Mungu Kwa Ulinzi ,Uzima na Nguvu , Kwa Taifa,familia , Makanisa, viongozi,Huduma,BiasharaKadiri Roho Mtakatifu atakavyokuongoza *Zaburi 92:1-2.*
✓ Omba Toba Na Rehema juu ya Makanisa, Familia ,Watoto , Nchi,Watumishi , ZABURI 51:4
✓Omba Utakaso Wa Nafsi, roho na Mwili . 1Wathesalonike 5:23.
1•Omba Bwana Akusaidie upate kibali machoni pake. omba neema iongezeke kwako, familia yako, katika huduma , biashara , kazi, elimu, nk. 2 Kor 12 : 9. Mwanzo 39 : 4..ombea na Wengine Kwa Hilo Hitaji.
2•. 1 Wakorintho 15 : 10. Niko hivi nilivyo kwa neema yako. Naomba kibali chako katika maisha yangu,. Naomba neema yako katika maisha yangu isiwe bure.ombea na Wengine .
3• Napokea kibali na milango itafunguka kuanzia sasa kwa Jina la Yesu .Dan 1 : 9.
• Kibali cha Bwana kifungue milango Ya Kazi,Elimu ,Biashara, Uongozi , Utumishi , iliyokua imefungwa katika jina Yesu.
• Kila mlima ulio simama mbele yangu na ung’oke kwa jina la Yesu. Zakaria 4: 6, Zaburi 84 : 11.
•Bwana wewe ni jua langu na ngome yangu,kila jambo jema litaachiliwa kwangu mwaka huu katika jina la Yesu.OMBEA NA WENGINE KWA HILO HITAJI.
4• Kama kanisa tusaidie kutembea katika neema yako,tupe neema ya kuongezeka,kuinuliwa na kupanda juu katika jina la Yesu. Zaburi 75 : 6.
Tamka Kanisa unaposalia, Na Usisahau na Kutaja Kanisa la Nuru Ya Upendo Neema Ya Mungu Ikawepo.
5•. Kwa neema yako dhambi haina nguvu juu yangu tena. Warumi 6 : 1-14. Warumi 7:1-23. Ombea na Wengine .
*N.B* Vipengele vya Maombi Mungu Akipenda Tutaona Kesho.
✍🏽 *NA IKIWA UNAHITAJI LAKO LA KUSHIRIKISHANA, MAOMBEZI, KUOKOKA, UKIONA AMANI TUMA. *_[Wagalatia 6:2]_* *Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.*
*_[Wakolosai 3:15 ]_* **Na amani ya Kristo iamue ndani yenu,ndiyo mliyo itiwa katika mwili mmoja* .
0793006146 .
✓Mungu akubariki.
🙏
❤️
👍
😋
😢
36