NURU YA UPENDO
NURU YA UPENDO
June 13, 2025 at 03:38 PM
*MAOMBI YA USIKU.* IJUMAA[13.06.2025]. JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO LIBARIKIWE SANA. KARIBU KATIKA MAOMBI YA USIKU VIPENGELE VITATUMWA KILA SIKU USIKU UNAOMBA WAKATI WA KULALA UKISHAMALIZA KULA CHAKULA CHAKO SIO MAOMBI YA MFUNGO. NENO KUU: Zaburi 27:4 "Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake." ✓ *VIPENGELE VYA MAOMBI YA LEO IJUMAA.TUNAOMBA* MAOMBI YA KUOMBEA WATOTO 👇👇.[Mithali 22:6, Zab 127:3, Mathayo 19:14. 1.Omba Ulinzi Wa Kimungu juu Ya Watoto Kwa Jina la Yesu. 2.Omba Neema Ya Mungu Juu Ya watoto. ■ Tamka maneno haya👇 ■ Nakushukuru Mungu Kwa Zawadi Ya Watoto ulionijalia [Taja majina yao....na Kama mmoja Taja Jina lake].Naomba Rehema Juu Ya Watoto na Utakaso , Nakukabidhi Maisha Yao , Afya zao, Akili zao na Ndoto zao Kwa Jina la Yesu Kristo, Walee Kwa Hekima yako, Wakujue wewe na kukutumikia katika Maisha Yao Yote , Walinde dhidi Ya Marafiki Wabaya, Tabia mbaya , Magonjwa na hila za adui Katika Maisha Yao.Wafunike Kwa Damu Yako Na Wajaze Na Roho wako Mtakatifu , Naomba Uwape Maisha Yenye Heshima ,Mafanikio,na Upendo Kwa Watu Wote Kwa Jina la Yesu Kristo.AMEN. *N.B* Vipengele vya Maombi Mungu Akipenda JUMATATU.16.06.2025. Itakuwa wiki Ya Maombi Ya makundi .Mfano tutaombea kundi la Wagonjwa, wazee, Vijana, Wamama., wababa , Watoto, Watumishi , Wanafunzi, Taifa, kadiri Roho Mtakatifu atakavyotoa Muongozo kwa hayo. ✍🏽 *NA IKIWA UNAHITAJI LAKO LA KUSHIRIKISHANA, MAOMBEZI, KUOKOKA, UKIONA AMANI TUMA. *_[Wagalatia 6:2]_* *Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.* *_[Wakolosai 3:15 ]_* **Na amani ya Kristo iamue ndani yenu,ndiyo mliyo itiwa katika mwili mmoja* . 0793006146 . ✓Mungu akubariki.
🙏 👍 21

Comments