
NURU YA UPENDO
June 16, 2025 at 03:25 PM
*MAOMBI YA USIKU.*
JUMATATU[16.06.2025].
JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO LIBARIKIWE SANA.
KARIBU KATIKA MAOMBI YA USIKU VIPENGELE VITATUMWA KILA SIKU USIKU UNAOMBA WAKATI WA KULALA UKISHAMALIZA KULA CHAKULA CHAKO SIO MAOMBI YA MFUNGO.
*NENO KUU* :YESU NI MPATANISHI NA MPONYAJI.
Isaya 53:5
"Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu;
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,
*Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona* ."
✓ *VIPENGELE VYA MAOMBI YA LEO JUMATATU.TUNAOMBA* MAOMBI YA KUOMBEA WAGONJWA👇👇.[
1.Maombi ya rehema na msamaha Kwa Wagonjwa .
●Omba Rehema na Toba kwa wagonjwa wote walioko Hospitalini na Sehemu Nyingine ata kama wewe ni Mgonjwa omba Rehema na Toba mbele za Mungu kama Unaweza Kuomba .
“Ee Bwana, unihurumie, unionyeshe nafsi, uniponye, kwa kuwa nimekutenda dhambi.” – Zaburi 41:4
2. Maombi ya faraja na nguvu kwa Wagonjwa .
●Omba Mungu Wagonjwa wote awape faraja , Nguvu hata wakati wa Mateso Na Damu Yake Ipite katikati Yao.
“Bwana humtegemeza mtu aliye kitandani mwa ugonjwa; Katika ugonjwa wake humfanyia tandiko lake.” – Zaburi 41:3
■Ondoa Vizuizi Vya uponywaji vilivyoshikilia Wagonjwa Kwa Jina la Yesu.
■kemea Roho za Wachawi zinazotuma Magonjwa na Madhahabu za ukoo hamisha kwa Jina La Yesu , Ukuta wa Laana uliowekwa Bomoa kwa Jina la Yesu .
■Kataa Magonjwa sugu, Magonjwa Ya Kurithi kwa Damu Ya Yesu ..Juu Ya Familia Yako, Juu Ya Watoto, n.k.
*N.B* : Vipengele vya Maombi vitatumwa Kesho.
✍🏽 *NA IKIWA UNAHITAJI LAKO LA KUSHIRIKISHANA, MAOMBEZI, KUOKOKA, UKIONA AMANI TUMA. *_[Wagalatia 6:2]_* *Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.*
*_[Wakolosai 3:15 ]_* **Na amani ya Kristo iamue ndani yenu,ndiyo mliyo itiwa katika mwili mmoja* .
0793006146 .
✓Mungu akubariki.
🙏
❤️
👍
👏
23