
NURU YA UPENDO
June 17, 2025 at 03:34 PM
*MAOMBI YA USIKU.*
JUMANNE[17.06.2025].
JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO LIBARIKIWE SANA.
KARIBU KATIKA MAOMBI YA USIKU VIPENGELE VITATUMWA KILA SIKU USIKU UNAOMBA WAKATI WA KULALA UKISHAMALIZA KULA CHAKULA CHAKO SIO MAOMBI YA MFUNGO.
*NENO KUU* : KUMJUA MUNGU.
Ayubu 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia."
✓ VIPENGELE VYA MAOMBI YA LEO JUMANNE.TUNAOMBA MAOMBI YA KUOMBEA VIJANA.
>Mshukuru Mungu Zab 118:1,21.
>Omba Toba na Rehema.
>Omba Utakaso Wa Nafsi. Roho na Mwili.
1.Omba Mungu Awape Neema Ya Wokovu Vijana Wapate kumjua Mungu Kwa viwango Vya Juu.
2.Omba Mungu alete utii Kwa vijana.1 Petro 5:5.
3.Omba mungu alete Hekima, .Maarifa na Ufahamu Kwa vijana .Daniel 1:4.
4.Omba Mungu Awatie Nguvu Vijana za Kusoma Neno lake Na Kuomba.1 Yohana 2:13-14.
5.Omba Mungu Awaepushe Na Majaribu Yanayotokana na Miili Pamoja na Tamaa Za Mwili Ikiwemo Uzinzi, Zinaa, Uasherati Na Ulevi.1 Kor :6:16
●Vunja Roho za wachawi Zinakwamisha Vijana Wasisonge Mbele kwa jina La Yesu.
● Ondoa Vizuizi Vya Maendeleo vinavyosimama kwa vijana kwa Jina la Yesu.
●Hamisha Madhahabu za Ukoo zinazoshikilia hatima , Bomoa Ukuta Wa kichawi, laana ,wivu na Kila maneno Yaliyotamkwa kwa vijana Yaondoe kwa Jina la Yesu.
*N.B* : Vipengele vya Maombi vitatumwa Kesho.
✍🏽 *NA IKIWA UNAHITAJI LAKO LA KUSHIRIKISHANA, MAOMBEZI, KUOKOKA, UKIONA AMANI TUMA. *_[Wagalatia 6:2]_* *Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.*
*_[Wakolosai 3:15 ]_* **Na amani ya KristoVipengele vya Maombi vitatumwa Kesho. iamue ndani yenu,ndiyo mliyo itiwa katika mwili mmoja* .
0793006146 .
✓Mungu akubariki.
🙏
👍
📘
😂
26