
JamiiCheck
May 24, 2025 at 01:41 PM
Taarifa zinazodai kuwa Dawa za Asili hazina Kemikali na kwamba ni salama kwa Asilimia 100 Si za Kweli
Kupitia Tafiti na Machapisho ya kitaaluma, JamiiCheck imebaini kuwa dawa zote zina Kemikali hata zile za Asili ambazo huwa na Kemikali asilia kutoka kwa mimea na wanyama.
Kemikali hizi zinaweza kuwa na athari chanya au hasi kwa afya ya binadamu. Mathalani Tanin inayopatikana kwenye baadhi ya mimea ina uwezo wa kuponya majeraha lakini pia inaweza kupelekea mwili kushindwa kufyonza Madini ya Chuma kama itatumika kwa kiwango kikubwa.
Soma https://jamii.app/DawaZaAsili

👍
🙏
3