
JamiiCheck
May 25, 2025 at 09:56 AM
JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa iliyochapishwa mtandao wa X ikidai Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, ameituhumu CHADEMA kuhusika na mauaji ya Ali Kibao Si ya Kweli.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu na marejeo ya video ya mkutano wa Askofu Gwajima Mei 24, 2025, hakutaja chama hicho kuhusika bali alikemea vitendo vya utekaji, akitumia tukio la Ali Kibao kama mfano.
Aidha, chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo limebainika kuwa la kughushi na halikutolewa na Millard Ayo.
Soma https://jamii.app/GwajimaMatukioUtekaji

👍
2