JamiiCheck

JamiiCheck

79.6K subscribers

Verified Channel
JamiiCheck
JamiiCheck
June 5, 2025 at 05:59 AM
Baada ya kurejea mahojiano ya Godbless Lema ya Juni 03, 2025, JamiiCheck imejiridhisha kuwa video inayochapishwa TikTok kuwa Lema amesema ''Gwajima alitakiwa kupewa kesi ya uhaini amefanya kitu kibaya'', imepotoshwa. Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa Video hiyo imehaririwa kwa kukata na kuunganisha vipande isivyostahili ili kupotosha ujumbe uliokusudiwa Katika mahojiano na Habari digital, Lema alisema "Kama maneno ya Gwajima ni 'strong' mpaka kanisa lifungwe, maana yake alitakiwa apewe kesi ya uhaini, Gwajima alikemea utekaji, mauaji na kutaja idadi ya waliotekwa, huyu mtumishi wa Mungu anasema haya mambo yakome" Soma https://jamii.app/LemaUhainiGwajima
❤️ 👍 🙏 3

Comments