
JamiiCheck
June 13, 2025 at 12:43 PM
Kwa kutumia Google Reverse Image Search na marejeo ya video, JamiiCheck imejiridhisha kuwa video inayodai Godbless Lema akuwataka Tundu Lissu na Heche wapumzike ni waropokaji, imepotoshwa.
Video hiyo imehaririwa kwa kukata na kuunganisha isivyofaa vipande vya hotuba ya Lema ya Januari 19, 2025, alipozungumza na viongozi wa CHADEMA ngazi za mikoa, ambapo alieleza kuwa walitaka Mbowe apumzike uongozi wa chama
Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutumia video ya zamani isivyostahili na kupotosha Uhalisia, hivyo hakikisha unathibitisha kwa kutafuta chanzo halisi cha Taarifa.
Soma https://jamii.app/LemaWaropokaji
👍
1