JamiiCheck
June 19, 2025 at 01:10 PM
Juni 19 ni Siku ya Selimundu (Sickle Cell) Duniani, ikilenga kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huu wa damu, changamoto za waathirika, na umuhimu wa elimu, upimaji wa vinasaba na huduma sahihi za afya.
Hata hivyo, kuna Taarifa Potofu nyingi kuhusu Selimundu zinazosababisha hofu na unyanyapaa, na kuwazuia watu kupata tiba sahihi.
Kama mdau wa JamiiCheck.com, tuambie ni dhana gani umewahi kusikia kuhusu ugonjwa huu ili tukusaidie kufahamu Uhalisia wake
Soma https://jamii.app/SikuYaSeliMunduDuniani
✨
1