
JamiiCheck
June 20, 2025 at 06:01 AM
Tafiti zinabainisha kuwa ukuaji wa Uume wa binadamu unategemea mifumo ya urithi na homoni maalum, na hauathiriwi kwa namna yoyote na kukatwa kwa Govi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), wanasisitiza kuwa tohara ina faida kiafya, kama vile kupunguza uwezekano wa kupata Saratani ya Uume na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hasa VVU/UKIMWI.
Tohara hufanyika kwa Watoto au Watu wazima, lakini Watoto hupona haraka zaidi kwa sababu bado hawajafikia umri wa hisia za kimapenzi.
Soma https://jamii.app/ToharaMwanaume

🇮🇷
😮
2