Economist SHILLA Jr.
June 15, 2025 at 06:08 AM
HALI YAKO YA MADENI IKOJE, JIBU MASWALI YAFUATAYO UWEZE KUJUA MADENI YAKO YAMEFIKIA HATUA GANI:
Kwa hali ya kawaida madeni yanapaswa kuwa himilivu kulingana na ukubwa wa KIPATO CHAKO. Uhimilivu wa madeni ni kwamba unaweza kurejesha MIKOPO au kulipa madeni yote bila kuathiri ubora wa maisha yako na familia yako. Ukitaka kubaini madeni yako yamefikia kiwango Cha kukutesa na kuathiri maisha yako kwa ujumla, jiulize maswali yafuatayo;
1. Madeni uliyonayo yanakufanya kukosa furaha?
2. Je, msukumo kutokana na madeni uliyonayo yanaathiri kazi yako na shughuli zako za kila siku?
3. Je, madeni uliyonayo yanaharibu heshima yako?
4. Je, madeni yanakufanya usijifikirie wewe zaidi?
5. Je, umewahi kutoa taarifa za uongo ili upate mkopo?
6. Je, umewahi kutoa ahadi zisizohalisi kwa wanaokukopesha?
7. Je, msukumo wa madeni uliyonayo yanakufanya kutokujali masuala ya familia yako?
8. Je, umewahi kuhofia mwajiri wako, familia yako au marafiki kujua kuhusu ukubwa wa madeni yako?
9. Ukiwa katika changamoto za kifedha, unajisikia ahueni zaidi juu ya kukopa?
10. Je, msukumo wa madeni uliyonayo yanasababisha kukosa usingizi?
11. Je, msukumo wa madeni uliyonayo yanasababisha kutumia pombe na madawa?
12. Je, umewahi kukopa pesa bila kujiridhisha vya kutosha kuhusu kiwango cha riba unayotakiwa kukopa?
13. Je, wakati wote unategemea tathmini hasi ukitakiwa kufanyiwa tathmini ya uwezo wako wa kukopesheka?
14. Je, umewahi kuweka ratiba ngumu kwa ajili ya kulipa madeni ili kuondokana na msukumo wa madeni?
15. Je, unaweza kutolea maelezo madeni yako na kujiambia mwenyewe kwamba una madeni mengi na kipindi ambacho ukiweza kurejesha madeni yataisha ndani ya kipindi kifupi?
KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI.
Book huduma zetu;
1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=);
2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=);
3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=)
4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo);
5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10);
Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].