
JamiiForums
June 20, 2025 at 01:27 PM
Kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Truth Social, Rais wa Marekani, Donald Trump ameandika "Siku nyingi za mapumziko zisizo za kazi nchini Marekani zinatugharimu mabilioni kwa sababu biashara nyingi hufungwa. Wafanyakazi nao hawapendi hali hiyo."
Trump ametoa kauli hiyo Juni 19, 2025, katika Sikukuu ya Kitaifa ya "Juneteenth" ambayo husherekewa Juni 19 kila Mwaka kwa ajili ya kuadhimisha kuachwa huru kwa Waamerika Weusi waliokuwa Watumwa
Trump ameongeza "Kwa mwendo huu tutakuja kuwa na sikukuu kila siku ya kazi. Hali hii lazima ibadilike kama kweli tunataka kuifanya Marekani kuwa na Nguvu tena." Pia Rais huyo hakuhudhuria wala kushiriki katika shughuli yoyote ya kuadhimisha sikukuu hiyo
Soma https://jamii.app/MapumzikoHugharimuMarekani

😂
😡
🖕
❤️
🏊♀
👍
👎
😮
🙏
🫴
18