
Legal Minds Forum ⚖️
June 9, 2025 at 04:17 PM
Update kutoka kwa _MENDEZ_
*KESI YA KANISA LA GWAJIMA: Serikali inasema haijafuta* Kanisa la Gwajima - *hakuna maamuzi ya kufuta* Kanisa la Gwajima linaloenda kwa *jina la Glory of Christ TANZANIA Church*. Na wala *Barua ya kufuta haijawahi kupelekwa kwenye Kanisa hilo.* Kwamba, *kinachoonekana kufutwa kwenye ile Barua* ya Msajili wa Jumuiya, *ni Kanisa linaloitwa Glory of Christ Church* (hakuna neno *TANZANIA*).
👆🏿 Kwahiyo, kwasababu *aliyeleta Maombi* ya Zuio na kutaka hali irudi kama ilivyokuwa _(status quo ante)_ *ni Glory of Christ TANZANIA Church* ambaye hakuna maamuzi ya kumfuta, *Serikali imeweka pingamizi* kwamba *Mahakama haina* mamlaka ya kusikiliza maombi hayo.
Kama ni hivyo👆🏿, *kwanini sasa Polisi walienda kwenye kanisa la Glory of Christ TANZANIA Church* kuzuia shughuli zisiendelee na kuwakamata Waumini *wakidai wanatekeleza Amri ya Msajili kulifunga kanisa hilo?* Ni hoja ya upande wa pili wakipinga pingamizi na kusema hiyo imewafanya wakate Rufaa kwa Waziri na kuleta maombi haya Mahakamani.
Mahakama Kuu imesema *haioni ni kwa namna gani Mamlaka yake yameporwa. Imetupilia mbali pingamizi.✍🏼*
_MD, Mendez (M.C.A)_
09/06/2025
👍
3