TRA TANZANIA

TRA TANZANIA

317.1K subscribers

Verified Channel
TRA TANZANIA
TRA TANZANIA
June 12, 2025 at 05:11 PM
#kigoma Leo tarehe 12 Juni 2025, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kigoma, Bw. Beatus Nchota, ametembelea Kiwanda cha Qilin Cement kilichopo mkoani Kigoma na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa kiwanda hicho, Bw. Fan Junping pamoja na watumishi wengine. Ziara hiyo imefanyika katika mwendelezo wa Kampeni ya Elimu na Utatuzi wa Changamoto za Kodi iliyoanzishwa rasmi tarehe 06 Juni, 2025 na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda sambamba na maadhimisho ya Alhamisi ya Kusikiliza Changamoto za Walipakodi. Katika ziara hiyo, elimu juu ya kodi mbalimbali kama vile VAT, PAYE, Income Tax na nyinginezo imetolewa ikiwemo kusikilizwa kwa changamoto zinazomkabili Mlipakodi na kupatiwa ufumbuzi.
Image from TRA TANZANIA: <a class="text-blue-500 hover:underline cursor-pointer" href="/hashtag...
🙏 👍 6

Comments