
TRA TANZANIA
June 17, 2025 at 10:08 AM
#njombe
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo 17 Juni, 2025 imeendelea na zoezi la utoaji elimu kwa Mlipakodi mlango la kwa mlango kwa Wafanyabiashara wa eneo la Mjimwema mkoani Njombe, ambapo wito mkubwa uliotolewa kwa wafanyabiashara hao ni kwenda kulipa kodi ya awamu ya pili inayoishia tarehe 30 Juni, 2025. Pia wamesisitizwa kutoa risiti za EFD kila wanapofanya mauzo au kutoa huduma. Aidha, Maafisa wa TRA wameendelea kutatua changamoto za Walipakodi mkoani hapo na kupokea maoni yao.
❤️
👍
😢
🙏
6