TRA TANZANIA

TRA TANZANIA

317.1K subscribers

Verified Channel
TRA TANZANIA
TRA TANZANIA
June 18, 2025 at 07:26 PM
TRA YAENDELEA NA KAMPENI YA ELIMU YA KODI NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO Naibu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa Bw. Gabriel Kimweri amesema amefarijika sana na ujio wa Watendaji wa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya mkoani Geita (GGM) katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kuwasilisha changamoto zao na kujadiliana mambo mbalimbali ya kodi. Ameyasema hayo leo tarehe 18.06.2015 katika Kikao ambacho ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi na kusikiliza changamoto yenye lengo kuwahudumia walipakodi kwa karibu zaidi na kutatua changamoto zao. Kwa upande wake Makamu wa Rais wa kodi wa Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya Ashanti ambayo ni Kampuni mama ya GGM na kiongozi wa ujumbe huo Bw. Gelishan Naicko amesema anaishukuru TRA kupitia Idara ya Walipakodi Wakubwa kwa ushirikiano wao wanaoendelea kuonesha jambo linalowasaidia wao kuendelea kulipa kodi zaidi na kwa wakati bila ya mgogoro wowote.
Image from TRA TANZANIA: TRA YAENDELEA NA KAMPENI YA ELIMU YA KODI NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO    ...
👍 3

Comments