Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
June 20, 2025 at 10:50 AM
TIA YAENDELEA KUTOA HUDUMA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 📍Chinangali, Dodoma 🗓️ 20 Juni 2025 Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) inaendelea kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2025. Ikiwa leo ni siku ya tano tangu kuanza kwa maadhimisho haya, TIA inaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, ikiwemo elimu kuhusu majukumu ya taasisi katika kutoa mafunzo ya kitaaluma kwenye nyanja za uhasibu, ununuzi na ugavi, pamoja na fani nyingine za biashara na utawala bora. Aidha, elimu juu ya huduma za ushauri wa kitaalamu na tafiti zinazolenga kuongeza tija katika sekta ya umma na binafsi inaendelea kutolewa kwa wageni wanaotembelea banda la TIA. Katika banda letu, tumeendelea kusisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni, taratibu na maadili ya utumishi wa umma, kwa lengo la kuimarisha misingi ya uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika utoaji wa huduma kwa wananchi. #dodoma2025 #wikiyautumishi #tiaelimukwaufanisi #tiatanzaniaupdates

Comments