Dr. BUDODI
Dr. BUDODI
June 16, 2025 at 04:07 PM
*UMRI UNAHUSIANA VIPI NA UTASA?* Kadri umri unavyoongezeka, idadi na ubora wa mayai kwenye ovari hupungua, hali inayoitwa Diminished ovarian reserve. Wanawake huzaliwa na mayai takriban milioni 1-2, lakini mpaka umri wa miaka 30, hifadhi hii inapungua hadi ~100,000, na chini ya 1,000 kwa miaka 40. Mayai yanayobaki mara nyingi huwa na kasoro, hasa baada ya miaka 35, ambazo hupunguza uwezekano wa kurutubishwa na hata yakirutubishwa husababisha mimba zenye kasoro. Homoni ya Anti-Müllerian Hormone (AMH) inapungua (chini ya 1 ng/mL baada ya miaka 35), na Follicle-Stimulating Hormone (FSH) huongezeka (>10 IU/L), zikionyesha mayai yanapungua. Umri ni sababu ya asili, lakini mambo kama maambukizi kwenye ovari, chemotherapy, au uvutaji sigara yanaweza kuharakisha upungufu wa mayai. Dalili zinaweza kujumuisha kubadilika kwa mizunguko ya hedhi, lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili hadi pale wanaposhindwa kupata ujauzito. Hali hii hugunduliwa kwa vipimo kinachoitwa Ovarian Reserve Test ambacho husaidia kuangalia kiwango na ubora wa mayai yaliyobaki. *INASABABISHAJE UGUMBA?* Umri unapunguza idadi na ubora wa mayai yanayopatikana kwenye ovulation, na mayai yanayobaki mara nyingi huwa na kasoro (mf, Down syndrome, hatari ya ~1% kwa miaka 35 ikilinganishwa na 0.1% kwa miaka 20). Hii hupunguza nafasi ya yai kurutubishwa na huongeza hatari ya kuharibika kwa mimba kwa ~20-50% baada ya miaka 35, ikiongezeka hadi ~90% kwa miaka 45. Mji wa mimba pia unakuwa mdhaifu ikipunguza ufanisi wa njia za kupandikiza, hasa baada ya miaka 40. *NJIA SALAAMA NA SAHIHI ZA KUBEBA MIMBA.* * _In Vitro Fertilization (IVF):_ Njia hii huhakikisha mayai machache yaliyobaki yanarutubishwa kiukamilifu na kupandikizwa kwenye kizazi. _* IVF kwa kuchangiwa mayai(Donor Egg IVF):_ inatumia mayai kutoka kwa mwanamke mwingine, hii hufaa zaidi ikiwa huna mayai kabisa. * _Ovarian Stimulation:_ Njia hii hutumia sindano za homoni kuamsha tena upevushaji wa mayai kabla ya kuingia kwenye IVF. *MAONI YA KITAALAMU* Ikiwa una zaidi ya miaka 35 na unashindwa kupata ujauzito baada ya miezi 6, au mwaka 1 chini ya miaka 35, wasiliana na Daktari mapema ambapo atapendekeza kipimo cha Ovarian Reserve Test (AMH, FSH, na ultrasound ya ovari) ili kuangalia hifadhi yako ya mayai. IVF ni chaguo la kwanza, lakini ikiwa mayai yako ni machache au ya ubora dhaifu, Donor Egg IVF inaongeza ufanisi. Usichelewe, kwani kila mwaka baada ya 35 hupunguza nafasi ya upandikizaji kufaulu. Epuka uvutaji sigara, pombe, na unene kwa kupunguza uzito (BMI 18.5-24.9) ili kuimarisha afya ya mayai. Daktari atakupa ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo wa kipindi cha matibabu. Kula chakula chenye vitamini D, omega-3, na folic acid kwa wingi ili kuimarisha afya ya uzazi. Kwa kuzingatia haya machache utaitwa mama hata ikiwa una umri mkubwa.

Comments