Dr. BUDODI
Dr. BUDODI
June 17, 2025 at 05:03 PM
MAGONJWA SUGU HUSABABISHA UTASA Mwili wako hufanya kazi kwa muumganiko maalumu unaotambulika kama Coordination mofumo tofauti ya mwili inaweza kutegemeana kwa namna tofauti na hivo mgumo mmoja ukiathirika na mwingine pia unaathirika. Hii ndio sababu kuu ya magonjwa sugu na magonjwa ya muda mrefu ambayo pengine hayana uhusiano wa moja kwa moja na mfumo wa uzazi kusababisha utasa. Magonjwa kama kisukari na hypothyroidism, huathiri 10-20% ya wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito. Bila matibabu ni vigumu kwa wenza wenye changamoto hizi kupata watoto. MAGONJWA SUGU HUATHIRI NINI HASA? Magonjwa ya muda mrefu ni hali zinazodumu kwa miaka, zikiathiri afya ya mwili kiujumla ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi. * Kisukari(diabetes) ambapo mwili huwa na viwango vya juu vya sukari, hii huiathiri upevushaji wa mayai na hupunguza uwezo wa mimba kutunga. * Hypothyroidism(tezi ya thairoidi 8isiyofanya kazi vizuri) hupunguza viwango vya homoni ya thyroid, na baadae zikisababisha kuvurugika kwa mizunguko ya hedhi na kudhoofisha upevushaji wa mayai. * Magonjwa ya kinga ya mwili(Autoimmune diseases) kama lupus hutoa kingamwili zinazoshambulia tishu za uzazi, zikiharibu mayai au mji wa mimba. * Magonjwa ya figo ya muda mrefu(chronic kidney disease) husababisha kupanda kwa viwango vya homoni zinazosababisha mwili kuvimba na kutengeneza michubuko,hali ambayo hupunguza ubora wa mayai. Sababu za magonjwa haya ni pamoja na kurithi, mtindo wa maisha (mf, lishe duni, unene au matumizi ya pombe na sigara). Dalili zinaweza kujumuisha hedhi zisizo eleweka, uchovu, maumivu ya viungo, au kushindwa kupunguza uzito, lakini utasa inaweza kuwa dalili ya kwanza. Hali hizi hugunduliwa kwa vipimo vya damu (mf, HbA1c kwa kisukari, TSH kwa thyroid) au vipimo vya ultrasound. *UTASA UNATOKEAJE?* Magonjwa ya muda mrefu yanazuia uzazi kwa njia mbalimbali. * Kisukari husababisha insulin resistance(homoni ya insulin kushindwa kufanya kazi), ikizuia upevushaji wa mayai na kuongeza hatari ya kuharibika kwa mimba kwa ~20-30%. * Hypothyroidism hupunguza homoni zinazohitajika kwenye upevushaji, ikisababisha hedhi kuvurugika na kupunguza uwezekano wa kupata ujauzito kwa ~15-25%. * Magonjwa ya kinga ya mwili(Autoimmune diseases) yanaweza kuharibu ovari, na kupunguza hifadhi ya mayai (AMH <1 ng/mL), au kuzuia mimba kutunga. * Ugonjwa wa figo husababisha sehemu za mwili kuvimba, ukipunguza ubora wa mayai na mji wa mimba, na kuongeza hatari ya matatizo ya uzazi kwa ~10-20%. *NJIA SALAMA ZA KUPATA MTOTO* * Matibabu ya Dawa: kama metformin (kwa kisukari) au levothyroxine (kwa hypothyroidism) hurejesha usawa wa homoni, ikiruhusu ovulation. * Intrauterine Insemination (IUI): Mbegu za kiume huingizwa kwenye kizazi wakati wa ovulation, njia hii hurahisisha urutubishaji na kutungwa kwa mimba. * In Vitro Fertilization (IVF): Mayai huritubishwa maabara na mtoto aliepatikana hupandikizwa kwenye kizazi, njia hii huepuka changamoto za kimaumbile kwa wanawake. *MAONI YA KITAALAMU* Ikiwa una kisukari, hypothyroidism, lupus, au ugonjwa wa figo na unashindwa kupata ujauzito, wasiliana na daktari ambapo atapendekeza vipimo vya damu (HbA1c, TSH, ANA) na ultrasound ya ovari ili kutathmini afya yako ya uzazi. Zingatia matibabu ya ugonjwa wako kwa kutumia dozi kikamilifu na badili mfumo wako wa maisha kwa matokeo mazuri zaidi ya njia za upandikizaji. Usichelewe, kwani umri zaidi ya 35 hupunguza ufanisi wa njia hizi. Punguza uzito ikiwa una zaidi ya kilo 75, epuka uvutaji wa sigara, na kula chakula chenye vitamini D, omega-3, na folic acid kwa wingi ili kupunguza adha ya sehemu za mwili kuvimba na kutengeneza michubuko. Daktari atakupa ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo kipindi cha matibabu. Ukizingatia machache haya na maelekezo mengine utakayopewa na daktari wako utapata mtoto.

Comments