Dr. BUDODI
Dr. BUDODI
June 19, 2025 at 06:17 PM
*KANSA INAATHIRI VIPI UZAZI?* Kansa ya mayai, kizazi, mlango wa kizazi na nyinginezo, huathiri moja kwa moja mfumo wa uzazi, ikipunguza ubora wa mayai au kuharibu mazingira ya mji wa mimba, matibabu ya kansa ndiyo yanayochangia zaidi kusababisha utasa. Chemotherapy hutumia dawa zenye sumu (k.m., cyclophosphamide) zinazoshambulia seli za kansa(hulenga seli zinazokua kwa kasi), zikiwemo seli za vifuko vya upevushaji. Hii hupelekea kuharibika kwa hifadhi ya mayai (AMH <1 ng/mL) na kusababisha premature ovarian Insufficient kwa 30-70% ya wagonjwa chini ya miaka 40. Radiotherapy(Mionzi) ya sehemu za nyonga (dozi >10 Gy) inaharibu mayai na mji wa mimba, ikipunguza idadi ya mayai na kufanya mji wa mimba kuwa dhaifu na kuzuia mimba kutunga. Vihatarishi ni pamoja na umri, wakati wa matibabu (zaidi ya miaka 30 hupunguza hifadhi ya mayai zaidi), aina ya dawa, na dozi ya mionzi. Dalili zinaweza kujumuisha hedhi kuvurugika, kukoma hedhi kabla ya miaka 40, au fukuto (hot flashes). Hali hizi hugunduliwa kwa vipimo vya kuangalia hifadhi ya mayai. *NAMNA INAVYOPELEKEA UTASA.* Chemotherapy inaharibu vifuko vya upevushaji mayai, ikipunguza idadi na ubora wa mayai, hali inayosababisha upevushaji(ovulation) kuwa wa kiwango cha chini au kukoma kabisa na kupunguza nafasi za ujauzito wa kawaida kwa ~50-80%. Radiotherapy kwenye nyonga inaharibu tishu za mji wa mimba, ikipunguza unene wa kuta za mji wa mimba(<7 mm) na kuongeza hatari ya kuharibika kwa mimba kwa ~30-50%. Kansa yenyewe, mf. kansa ya mayai, inaweza kuharibu hifadhi ya mayai, na kansa ya kizazi inaweza kuhitaji kuondolewa kwa mji wa mimba(hysterectomy), ikifanya ujauzito wa kawaida usiwezekane. *NJIA SALAMA ZA KUPATA MTOTO.* * IVF kwa kuchangiwa mayai (Donor Egg IVF); Hii hutumika ikiwa mayai ya mhusika yameharibika, ambapo mwanamke mwingine huchangia mayai. * Kuhifadhi Mayai (Egg Freezing); Kabla ya kuingia kwenye chemotherapy au radiotherapy mayai huvunwa na yatahifadhiwa kwaajili ya kutumika kwenye IVF baadae. Njia hii huyakinga mayai dhidi ya madhara ya tiba. * Surrogacy(Mama wa kujitolea) inatumika ikiwa mji wa mimba umeharibika, ambapo mwanamke mwingine hubeba mimba. * In Vitro Fertilization (IVF); Njia hii inaweza fanyika ikiwa hata baada ya matibabu kizazi na mayai viko salama. *MAONI YA KITAALAMU.* Ni vema kuwasiliana na daktari wa uzazi mara baada ya kugundulika una kansa yeyote mwilini. Daktari atapendekeza uhifadhi mayai kadhaa kabla ya kuanza tiba ya mionzi au chemotherapy. Hii itaongeza uwezekano wa kuzaa baadaee. Ikiwa tayari unapokea matibabu ya saratani au umepona, daktari atapendekeza vipimo vya AMH, FSH, na ultrasound ili kutathmini hifadhi yako ya mayai na ubora wa mji wako wa mimba. Donor Egg IVF ni chaguo bora ikiwa mayai yako yameharibika, na surrogacy inafaa ikiwa uterasi haiwezi kubeba mimba. Usichelewe, kwani umri zaidi ya miaka 35 hupunguza ufanisi wa njia hizi. Linda afya yako kwa chakula bora, epuka uvutaji sigara, na punguza uzito (BMI 18.5-24.9) ili kuimarisha njia za upandikizaji. Daktari atatoa ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia kukabiliana na msongo wa mawazo kipindi chote cha matibabu. Kula chakula chenye vitamini D, folic acid, na omega-3 kwa wingi ili kuboresha afya ya uzazi.

Comments