Mwanzo TV
June 18, 2025 at 12:11 PM
#tanzania: *AU YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI TANZANIA*
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amekutana na Misheni Maalum ya Umoja wa Afrika ya Kutathmini Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, na kuahidi kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa haki, uhuru na amani.
Misheni hiyo ya tathmini kabla ya uchaguzi (Pre-election Assessment Mission – PAM), iliyoongozwa na Dk. Phumzile Mlambo-Ngcuka, Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, iliwakilishwa na wajumbe 16, na ilifanya mazungumzo na Waziri Mkuu jana Juni 17, 2025 katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam