Mwanzo TV
Mwanzo TV
June 18, 2025 at 01:11 PM
#geneva: *POSSI: SERIKALI YA TANZANIA INACHUKULIA KWA UZITO MATUKIO YA UTEKAJI* Seikali ya Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kulinda na kuendeleza haki za binadamu, utawala bora na utawala wa sheria kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025. Kauli hiyo imetolewa na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Dkt. Abdallah S. Possi, wakati wa majadiliano ya wazi kuhusu taarifa ya mwaka ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza kwa niaba ya Tanzania, Dkt. Possi alieleza kuwa serikali imejizatiti kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, uwazi, na kwa kuzingatia viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa vya haki za binadamu. “Tanzania inaendelea kulinda uhuru wa kujieleza, haki ya kupata taarifa, na ushiriki wa vyombo vya habari. Tunaamini katika usawa mbele ya sheria kwa watu wote, wakiwemo watetezi wa haki za binadamu,” alisema Dkt. Possi.
Image from Mwanzo TV: <a class="text-blue-500 hover:underline cursor-pointer" href="/hashtag...

Comments