Mwanzo TV
Mwanzo TV
June 18, 2025 at 01:15 PM
#geneva: *BALOZI POSSI:MWANGI NA AGATHA WALIKIUKA SHERIA ZA UHAMIAJI TANZANIA* Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Dkt. Abdallah S. Possi, wakati wa majadiliano ya wazi kuhusu taarifa ya mwaka ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, akizungumza kwa niaba ya Tanzania, Kuhusu tukio la hivi karibuni linalowahusisha watetezi wa haki za binadamu kutoka nje ya nchi, Boniface Mwangi kutoka Kenya na Agatha Atuhaire kutoka Uganda, alieleza kuwa Wanaharakati hao walirudishwa makwao baada ya kukiuka sheria za uhamiaji. Balozi Possi alisisitiza kuwa, kwa mujibu wa sheria, wageni wote wanatakiwa kutoa sababu halali na za kweli za kuingia nchini. “Kuwa mtetezi wa haki za binadamu hakumfanyi mtu kuwa juu ya sheria za nchi nyingine. Heshima kwa sheria ni msingi wa ushirikiano wa kimataifa,” aliongeza.
Image from Mwanzo TV: <a class="text-blue-500 hover:underline cursor-pointer" href="/hashtag...

Comments