
Mwanzo TV
June 18, 2025 at 03:38 PM
#marekani: *TYLER PERRY ASHTAKIWA KWA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO*
Tyler Perry, mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, mwandishi wa michezo ya kuigiza, na mkurugenzi kutoka Marekani anakabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono iliyofunguliwa na muigizaji Derek Dixon, ambaye alishiriki katika tamthilia yake ya 'The Oval'.
Mashtaka hayo yanaeleza matukio kadhaa, ikiwa ni pamoja na madai kwamba Perry alimshika Dixon kwa nguvu, alitoa maombi yasiyofaa, na kumshinikiza katika hali zisizotakikana.
Dixon pia anadai kwamba Perry alimtishia kuhusu hatima ya mhusika wake katika The Oval, akimpa ishara kwamba nafasi yake ingeondolewa ikiwa hatakubaliana na matakwa yake.
Timu ya wanasheria wa Perry imekanusha vikali madai haya, ikiyaita "ya kutungwa" na kuielezea kesi hiyo kama "njama ya kumharibia jina"
