Mwanzo TV
Mwanzo TV
June 19, 2025 at 12:14 PM
#kenya: *MAAFISA 2 WALIOHUSIKA KUMPIGA RISASI MCHUUZI WA BARAKOA NAIROBI WAZUILIWA KWA SIKU 15* Mahakama ya Nairobi imeamuru kuzuiliwa kwa maafisa wa polisi Masinde Barasa na Duncan Kiprono kwa siku 15 huku uchunguzi ukiendelea kuhusu kupigwa risasi kwa mchuuzi Boniface Kariuki wakati wa maandamano ya Juni 17. Maafisa hao wawili, walionaswa kwenye video wakidaiwa kumpiga risasi Kariuki karibu na barabara ya Moi, walifikishwa katika Mahakama ya Milimani mnamo Alhamisi Juni 19. Mahakama iliipa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) muda wa kukamilisha uchunguzi wao. Kariuki, ambaye alikuwa akiuza barakoa, bado yuko katika chumba cha watu mahututi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. Kufikishwa kwao tena mahakamani kumepangwa Julai 3, mahakama itakapokagua maendeleo ya upelelezi.
Image from Mwanzo TV: <a class="text-blue-500 hover:underline cursor-pointer" href="/hashtag...

Comments