
Mwanzo TV
June 20, 2025 at 11:09 AM
#kenya: *POLISI MUKHWANA KUSHIKILIWAN KWA SIKU 21 KUPISHA UCHUNGUZI ZAIDI YA MAUAJI YA MWALIMU OJWANG*
Polisi Konstebo James Mukhwana ameagizwa kusalia rumande kwa siku 21 huku uchunguzi ukiendelea kuhusu kifo cha mwanablogu na mwalimu Albert Ojwang’, ambaye alifariki katika hali tatanishi mikononi mwa polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Central jijini Nairobi, nchini Kenya.
Katika taarifa ya kina, Mukhwana aliripotiwa kumhusisha mkuu wake, OCS Samson Talaam, akidai alimuelekeza kuwaagiza wafungwa kumuadhibu Ojwang', agizo linalodaiwa kuwa lilitoka kwa Naibu Inspekta Jenerali Eliud Lagat.
Mahakama iliipa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) muda zaidi kukamilisha uchunguzi wao, ikitaja madai mazito ya utovu wa nidhamu wa polisi.
