
Mwanzo TV
June 20, 2025 at 01:37 PM
#zambia: *MAZISHI YA RAIS WA ZAMANI WA ZAMBIA, DKT. LUNGU, KUFANYIKA AFRIKA KUSINI*
Familia ya hayati Rais wa zamani wa Zambia, Dkt. Edgar Lungu, imethibitisha kuwa mazishi yake yatafanyika kwa ibada ya faragha nchini Afrika Kusini, ambako alifariki dunia tarehe 5 Juni 2025 akiwa na umri wa miaka 68.
Taarifa kutoka kwa msemaji wa familia, wakili Makebi Zulu, zinaeleza kuwa Lungu aliacha maagizo maalum kabla ya kifo chake, ikiwa ni pamoja na kutaka Rais wa sasa, Hakainde Hichilema, asihusishwe kwa namna yoyote na shughuli za mazishi yake.
Hii imezua mvutano mkubwa kati ya familia, serikali, na chama chake cha zamani, Patriotic Front, kuhusu mipango ya maziko.
Hata hivyo, kufikia katikati ya Juni, familia na serikali walifikia makubaliano: mwili wa Lungu utasafirishwa kutoka Afrika Kusini hadi Lusaka kwa ndege ya kukodi, na mazishi ya kitaifa yamepangwa kufanyika Jumapili, Juni 22, 2025, huku wananchi wakipewa nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kuanzia Alhamisi.
