
Mwanzo TV
June 20, 2025 at 03:01 PM
#iran: MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA TEHRAN KULAANI MASHAMBULIZI YA ISRAEL
Maandamano makubwa yamefanyika jijini Tehran na miji mingine ya Iran kama Tabriz na Shiraz, ambapo maelfu ya wananchi waliandamana kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya miundombinu ya Iran, hasa maeneo yanayohusishwa na mpango wa nyuklia.
Waandamanaji walionekana wakiwa na mabango, picha za makamanda waliouawa, na bendera za Iran pamoja na Hezbollah.
Wengi walikusanyika baada ya sala ya Ijumaa, wakitoa kauli za kuunga mkono serikali na kiongozi wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei.
Maandamano kama haya pia yameripotiwa Beirut (Lebanon) na Baghdad (Iraq), yakionyesha mshikamano wa kikanda dhidi ya hatua za kijeshi za Israel.
