Duro Crypto
Duro Crypto
June 13, 2025 at 04:12 PM
*Historia ya Bei ya Bitcoin* *Tupate Overview kidogo* Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, safari ya Bitcoin imekuwa na misukosuko mingi, bei inapanda na kushuka kutokana na mambo ya kisiasa, hali ya uchumi duniani, na mabadiliko ya kisheria. Bei ya Bitcoin ilianzia dola dola 0.30 mwaka 2011 hadi kufikia kiwango cha kihistoria cha dola111,980 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 37,000,000 kwa chini ya miaka 14. Kuanzia 2020 bei ya chini kabisa ikiwa ni dola 3,880 hadi bei ya juu kabisa 2025 ya dola 111,980, Bitcoin ilipanda kwa zaidi ya asilimia 2,700. Kuanzia 2011 hadi 2025, Bitcoin imekuwa ikileta wastani wa faida ya asilimia 142 kila mwaka. Kufikia tarehe 10 Juni 2025, thamani ya jumla ya soko la Bitcoin ni takriban dola trilioni 2.18, na inachukua asilimia 64 ya soko zima la crypto. *Twende kazi* 👇 Bitcoin (BTC) imekuwa ikivuta hisia za watu duniani kote kutokana na thamani yake kupanda kwa kasi ya ajabu tangu mwaka 2009. Lakini haikuwa rahisi, imepitia nyakati ngumu, kuporomoka kwa bei, na hata bear markets za muda mrefu. Pamoja na kutokuwa na utulivu, Bitcoin mpaka sasa imefanya vizuri kuliko mali nyingine yeyote ya kawaida. Mambo mengi huathiri bei ya Bitcoin, na kuna njia tofauti za kuchambua historia yake ya bei.
Image from Duro Crypto: *Historia ya Bei ya Bitcoin*    *Tupate Overview kidogo*   Tangu kuanz...

Comments