Duro Crypto
Duro Crypto
June 13, 2025 at 05:06 PM
*Jinsi ya Kuchambua Historia ya Bei ya Bitcoin* Kuna njia kuu tatu: 1. *Technical Analysis (TA)* – Kuangalia bei na kiasi cha mauzo yaliyopita kutabiri mwenendo wa baadae. Mfano, kutumia moving averages kama ile ya siku 50 (50-day SMA) kuangalia kama bei ina nguvu au dhaifu 2. *Fundamental Analysis (FA)* – Kuchunguza thamani halisi ya mradi kama Bitcoin, kama vile idadi ya watumiaji wa kila siku, miamala, au maendeleo ya kiufundi yanayoonyesha uwezo wa muda mrefu. 3. *Sentiment Analysis (SA)* – Kutazama hisia za watu kuhusu soko, kama watu wengi wanasema maneno mazuri kuhusu Bitcoin mitandaoni, basi mara nyingi bei hupanda kwa sababu ya matarajio chanya. *Biashara za Mwanzo za Bitcoin* Mwaka 2009, Bitcoin ilikuwa inajulikana na watu wachache sana. Ilikuwa inauzwa kwa makubaliano binafsi (OTC) kupitia majukwaa kama BitcoinTalk. Satoshi Nakamoto alichimba block ya kwanza Januari 3, 2009, na kutuma Bitcoin 10 kwa Hal Finney siku 9 baadaye hii ndiyo ilikuwa muamala wa kwanza kabisa wa Bitcoin. Tarehe 22 Mei 2010, mtu aitwaye Laszlo alinunua pizza mbili kwa kutumia Bitcoin 10,000, muamala huu wa kihistoria unaadhimishwa kila mwaka kama “Bitcoin Pizza Day”. Mwaka 2011, bei ilifika $0.30, na ndipo sekta ya crypto ilianza kuvutia watu zaidi, japo bado haikuwa na udhibiti wowote rasmi. Hii pia ilisababisha matukio ya kudukuliwa kwa masoko na kuporomoka kwa bei.

Comments