
Duro Crypto
June 13, 2025 at 05:57 PM
*Nini Hufanya Bei ya Bitcoin Kupanda au Kushuka?*
1. *Ugavi na Mahitaji* : Kuna Bitcoin milioni 21 tu zitakazowahi kuwepo. Kadri watu wanavyokubali kuitumia, mahitaji yanapanda lakini ugavi ni mdogo hii husababisha bei kupanda.
2. *Sheria na Udhibiti:* Serikali zinavyozidi kuelewa teknolojia ya crypto, zinatoa sheria mpya, wakati mwingine zinasaidia soko kukua, wakati mwingine husababisha wasiwasi na bei kushuka.
3. *Hali ya Uchumi Duniani:* Mambo kama mfumuko wa bei, viwango vya riba, au sera za fedha za serikali huathiri hisia za wawekezaji kuhusu Bitcoin.
4. *Gharama ya Uzalishaji (Mining):* Kuchimba Bitcoin kunahitaji umeme mwingi na vifaa vya gharama kubwa. Gharama hizi huweka kiwango cha chini cha bei, bei ikiwa chini ya gharama, wachimbaji wanapata hasara.
*Historia Fupi ya Bei ya Bitcoin*
2011: $0.30
2025: $111,980
Toka dola 3,880 mwaka 2020 hadi dola 111,980 mwaka 2025 ni sawa na ongezeko la zaidi ya 2,700%
Faida ya wastani kwa mwaka (2011-2025): 142%
Juni 2025: Thamani ya soko ni $2.18 trilioni na inachukua asilimia 64 ya soko lote la crypto.