
Duro Crypto
June 21, 2025 at 03:47 AM
*SCALP TRADING NI NINI?*
_Kwa ufupi kabisa_
Scalp trading ni kufanya biashara ya ku-buy na ku-sell kwa haraka sana ili kupata faida ndogo ndogo, mara nyingi kwa siku. Mfanyabiashara anaweza kufanya trade hata 50 au zaidi kwa siku moja.
Mfano, Ni kama kununua bidhaa Kariakoo asubuhi kwa elfu 10 na kuiuza jioni hiyo hiyo kwa elfu 12 Una faida ya buku mbili. Ukifanya hivyo mara nyingi kwa siku, hela inaongezeka na kuwa nyingi
*Je hii inawafaa kina nani?*
Watu wanaopenda kuangalia chati kila wakati
Wanaopenda kuingia na kutoka kwenye biashara haraka
Wenye utulivu wa akili, nidhamu, na uelewa wa masoko
*Lengo la Scalper ni Nini?*
Sio kupata faida kubwa mara moja, bali faida ndogo ndogo mara nyingi.
Mfano: Unanunua Bitcoin kwa Tsh 160M, unauza baada ya dakika kwa 160.1M. Faida ni laki moja. Ukirudia hivyo mara 10 kwa siku, unapata millioni moja.
