
Duro Crypto
June 21, 2025 at 04:03 AM
*Hatari Zake ni Zipi?*
1. *Kupoteza haraka* : Bei inabadilika ghafla sana, ukiingia vibaya unapoteza.
2. *Inahitaji kuwa macho muda wote:* Huwezi kwenda kumsalimia jirani wakatu huku uko kwenye trade.😀
3. *Inachosha kichwa:* Huwa inahitaji maamuzi ya haraka haraka, presha pia ni kubwa.
4. *Ada nyingi:* Kila unavyofanya trade kuna ada ya platform, ikizidi huwezi kuona faida.
5. *Mashindano na bots: Kuna mashine* zinazofanya hizi trades kwa sekunde, ni ngumu kushindana nazo kwa mikono.
*Timeframe*
Scalpers hutumia timeframe ndogo kama dakika 1, dakika 5 au dakika 15. Wengine hata hutumia sekunde 15, lakini hapa wanakutana na bots.
Mara nyingi, scalper huanza kwa kuangalia timeframe kubwa (kama saa 1 au siku 1) ili kujua mwelekeo wa soko, kisha huingia timeframe ndogo kutafuta fursa.
*Technical Analysis kwa Scalping*
Scalping inategemea sana technical indicators. Scalpers huangalia:
Candlestick patterns
Moving Averages
RSI
Bollinger Bands
VWAP
Fibonacci retracement
MACD
Wengine hutumia order book, volume profile, open interest, na wengine hutengeneza indicators zao wenyewe.