IAA Tanzania

IAA Tanzania

24.0K subscribers

Verified Channel
IAA Tanzania
IAA Tanzania
May 31, 2025 at 08:54 PM
IAA YASHIRIKI HANANG' MARATHON 2025 Washiriki kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), leo wameungana na washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini kushiriki mbio fupi (Hanang' marathon-Mount Hanang Adventure 2025) mwaka 2025 iliyofanyika kwa mara ya kwanza ndani ya hifadhi ya Mlima Hanang'. Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mlima Hanang' Abubakar Mpapa amesema lengo la mbio hizi ( kilomita 15 na kilomita 7) ni kuendelea kuunga mkono juhudi za utunzaji na uhifadhi wa mazingira. Aidha, Mhifadhi Mkuu Bwn. Mpapa ameushukuru Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)kwa kudhamini 'marathon' hii ya kwanza na kuomba uendelee kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira. Mlima Hanang ni mlima mrefu wa Nne Tanzania baada ya mlima Kilimanjaro, Meru, Lolmalasin wenye mita 3,423. Upekee wa mlima huu ni jinsi ulivyo mandhari nzuri na uoto wa asili wa kipekee.

Comments