IAA Tanzania

IAA Tanzania

24.0K subscribers

Verified Channel
IAA Tanzania
IAA Tanzania
June 2, 2025 at 03:03 PM
WANAFUNZI IAA WAPEWA MAFUNZO YA KUKUZA BIASHARA StarHubAfrica kwa kushirikiana na Benki ya CRDB wametoa mafunzo ya siku mbili mwishoni mwa wiki kwa wanafunzi zaidi ya 200 wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA ) walio chini ya Kiatamizi( IAA Business Start up Centre). @bsuc_iaa Mafunzo hayo yalilenga kuwapa wanafunzi na wajasiriamali wa hatua za awali ujuzi wa kuanzisha na kukuza biashara pamoja na stadi za kifedha. Katika mafunzo hayo wanafunzi walijifunza namna ya kubadilisha wazo kusa biashara hai, kuchambua fursa za masoko na kufanya utafiti wa kupitia mahojiano ya moja kwa moja. Aidha, walijifunza kuhusu uelewa wa fedha binafsi, mbinu bora za usimamizi wa fedha, tathmini ya uhalisia wa fedha katika biashara pamoja na hatua mbalimbali za safari ya uanzishaji wa biashara. Pamoja na mafunzo haya, wanafunzi hao wataendelea kunufaika kupitia ushauri wa miezi mitatu, ambapo wataunganishwa na wajasiriamali waliopo hatua za mbele wakifungua milango ya ushirikiano, kujifunza na kukuza biashara zao kwa pamoja. Wanafunzi 30 kati ya 200 waliopata mafunzo wanatarajiwa kushiriki mashindano ya kupata mtaji wezeshi wa kuanzia. #starthubafrica #crdbbank #iaanextlevo

Comments