
IAA Tanzania
June 11, 2025 at 07:40 AM
DIPLOMA IN ECONOMICS AND FINANCE
➡️ Wanafunzi wanaochagua kozi hii wanatarajiwa kunufaika na uwezo wa kufikiri kwa upande wa kifedha, ujuzi wa kihisabati, na ufahamu wa taasisi unaohitajika kutatua matatizo yanayotokea katika fedha na uchumi.
➡️ Kozi hii itawapa wanafunzi maarifa ya kisayansi juu ya michakato ya kifedha kwa ajili ya maendeleo na haswa, kutumia maarifa hayo katika kutathmini taasisi za kiuchumi na kifedha.
➡️ Wanafunzi wataweza kuchambua masuala mbalimbali ya kiuchumi na kifedha na kuelewa misingi ya sera za kiuchumi.
➡️ Kozi hii inamuandaa kijana kujiajiri au kuajiriwa katika fani za uchumi, fedha, Benki na hata katika biashara.
➡️ Vilevile inamuandaa kijana Kusoma ngazi ya degree katika fani mbalimbali za Mambo ya uchumi, uhasibu, fedha na benki.
➡️ Kozi hii inapatikana katika Kampasi ya Arusha.
➡️ Sifa za kujiunga
DIPLOMA YA MIAKA MIWILI
NTA Level 4: GPA ya 3.0 kutoka chuo kinachotambulika
Form Six: D moja na S
DIPLOMA YA MIAKA MITATU
Form Four: Angalau D nne
➡️ Kujiunga apply Online, Link Iko kwenye post au tuma ujumbe mfupi kwa text, WhatsApp, Kupitia namba 0742833444
Karibu sana IAA.
#iaanextlevo
👍
❤️
7