
IAA Tanzania
June 18, 2025 at 07:50 PM
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimeendelea kutoa mafunzo ya maadili na uadilifu kwa viongozi wakuu wa taasisi mbalimbali za umma nchini kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Lengo ni kuona mabadiliko halisi katika namna viongozi wanavyotekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, uwajibikaji na uongozi bora.
Leo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Moses Pesha amefunga mafunzo yaliyofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 18 Juni, 2025, katika Hoteli ya Corridor Spring jijini Arusha.
👍
3