
IAA Tanzania
June 19, 2025 at 07:43 AM
DIPLOMA YA CLEARING AND FORWARDING MANAGEMENT
➡️ Katika mazingira ya sasa ya kiuchumi, soko na mahitaji ya baadaye yanahitaji wahitimu wenye uwezo wa kitaalam wa kuunganisha huduma za bandari na usimamizi wa Forodha na Usafirishaji.
➡️ Kozi hii itawawezesha wahitimu kupata uelewa, maarifa na ujuzi wa kina kuhusu biashara ya kimataifa uliounganishwa na stadi za usimamizi wa bandari, ili waweze kuwa na mchango chanya katika mazingira ya kisasa ya kibiashara.
➡️ Kozi hii itawaandaa wahitimu waliobobea na wenye uelewa sahihi, ujuzi na uwezo wa kusimamia masuala ya bandari pamoja na Forodha na Usafirishaji, ili waweze kung’ara katika mashirika ya kibiashara ya ndani na ya kimataifa, pamoja na shughuli binafsi.
➡️ Wahitimu wa programu hii watakidhi mahitaji ya sasa ya soko la ajira, au kuanzisha shughuli zao binafsi za kibiashara katika mazingira ya kisasa.
➡️ Kozi hii inapatikana katika Kampasi ya Arusha.
----
➡️ Sifa za kujiunga
Form Six: D moja na S (kozi miaka miwili)
Form Four: D nne (kozi miaka mitatu)
➡️ Kujiunga jaza fomu online, link ipo kwenye tangazo. Au tuma ujumbe kwa simu namba 0742833444
#iaanextlevo

👍
🙏
4