
Bado nature visuals 📸
June 6, 2025 at 04:29 PM
*Upweke*
*Nimesimama peke yangu* …
Si kwa sababu wamenisahau,
Bali kwa sababu nimejifunza kuchanua katika kimya.
*> Naiona dunia ikipita mbele yangu.*
Nayasikia maisha wakiwa mbali na mimi —
Kicheko nisichokicheka,
Nyimbo nisizoiimba pamoja nao.
*> Lakini katika utulivu huu... nimemjua nafsi yangu* .
Katika upepo unaovuma, nimesikia jina langu.
> **Ninalia… si kwa uchungu* ,*
Bali kwa uzuri ambao hakuna anayesimama kuuona.
> *Wanafikiri niko mpweke* …
Lakini ukweli ni kwamba, mimi ni huru.
📸Bado Nature Visuals
🖊️ M. Kupa
📍Mahale Mountains National Park.

❤️
😂
5