
Wizara ya Afya Tanzania
June 17, 2025 at 05:10 AM
KUJENGEWA UWEZO MADAKTARI NA WATOA HUDUMA MKOANI GEITA KUTAONGEZA UFANISINA UBORA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Na WAF - GEITA
Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Geita Hermani Matemu amesema licha ya wananchi wa Mkoa huo kunufaika na Huduma za kibingwa kwa ukaribu na kwa gharama nafuu lakini pia kujengewa uwezo kwa wataalamu na watoa huduma katika mkoa huo kutasaidia kuzidi kuimarika kwa hali ya utoaji na Ubora wa huduma kwenda sambamba na nia ya Mhe. Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora.
Bw. Matemu ameyasema hayo Julai 16, Mkoani Geita wakati wa Mapokezi ya Madaktari bingwa wa Rais Samia ambao watakua mkoani hapo kwa Muda siku 7 kutoa huduma za Afya kibingwa Mkoani hapo.
“Wananchi wetu watapata kile ambacho wanakitaka, mtaweza kuwajengea wataalamu ili baada ya nyie kuondika wananchi waendelee kupata huduma na itasaidia japokua itakua sio kwa kiwango kile mnachotoa nyinyi lakini tija itakuwepo” amesema Matemu.
Nae Mratibu wa zoezi la Madaktari bingwa wa Rais Samia kwa mkoa wa Geita Paskalina Endrew kutoka wizara ya afya amesema lengu kuu la zoezi hili kuwasogezea wananchi huduma za kibingwa na bobezi na kuwajengea uwezo watoa huduma katika maeneo yao ya kazi.
Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt. Stephen Mwaisobwa pamoja na Dkt. Neveline Mwakaboko mganga mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale wamewataka wananchi wenye uhitaji wa matibabu ya kibingwa kujitokeza kwenye hosptali za wilaya zilizopo kila halmashauri ili kupata huduma ya matibabu.

❤️
🙏
3