Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
June 17, 2025 at 07:57 AM
WAMILIKI NA WATAALAMU WA MAABARA BINAFSI ZA AFYA WAHIMIZWA KUTOA HUDUMA KWA KUFUATA TAALUMA NA MAADILI. Wataalamu wa Maabara za Afya wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni zinazosimamia uendeshwaji wa Maabara hizo ili kutoa huduma bora kwa jamii. Hayo yamesemwa Juni 16,2025 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wamiliki wa Maabara Binafsi za Afya na wataalamu wa Maabara uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa jijini Dodoma. Amesema wataalamu wa maabara ni wadau muhimu kwani wanafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari ilikuweza kutambua magonjwa mbalimbali kwa kufanya vipimo na kutoa majibu sahihi kwa wagonjwa na sio vinginevyo. “Lengo la maabara ni uchunguzi kulingana na maelezo ya mgonjwa na sio kufuta mapato/maslahi, kwa mfano mtu anasema anaumwa mguu huku unampima UTI kwasababu unamaslahi labda ya dawa au maelekezo mengine ya kimapato hivyo sio maadili ya kazi yako.” Amesema Bw. Mmuya Amewataka pia wanataaluma kukaa kwenye taaluma na kuifanyia kazi miiko ya taaluma yao. Aidha amesisitiza kuwa kila mtumishi afanye kazi kwa kufuata taaluma aliyoisomea ili kuweza kutoa huduma nzuri na yenye viwango kwa wananchi. “ Wagonjwa wakifika hospitalini hawajui nani ni nani wakiona tu umevaa koti jeupe wanajua ni daktari, sasa baadhi ya wanataaluma wa Maabara wanauvaa uhusika wa udaktari wakati wanajua sio madaktari hivyo nawasihi mfanye kazi kwa taaluma mliyosomea” amesema Bw. Mmuya Aidha Bw. Mmuya ametoa rai kwa wamiliki wa Maabara binafsi kuhakikisha Maabara zinakuwa na vitu vyote muhimu kulingana na miongozo inavyohitaji. “Majengo yawe na sifa za kutoa huduma husika, kulingana na miongozo, hii itasaidia kutoa huduma bora na mazingira mazuri lakini kinyume chake kutaleta shida kwa wagonjwa wakati wa kupata huduma.” amesema Bw. Mmuya Naye mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Thomas Rutachunzibwa amewaasa watendaji wa maabara kuhakikisha wanatoa majibu sahihi na kufuata miiko ya kazi.
Image from Wizara ya Afya Tanzania: WAMILIKI NA WATAALAMU WA MAABARA BINAFSI ZA AFYA WAHIMIZWA KUTOA HUDUM...
❤️ 👍 😢 😌 20

Comments