Wizara ya Afya Tanzania
                                
                                    
                                        
                                    
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                June 17, 2025 at 12:59 PM
                               
                            
                        
                            WAZIRI MHAGAMA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA 
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ametekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutembelea majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea Meatu Mkoani Simiyu waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda BUGANDO Mkoani Mwanza ambao wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya awali. 
Waziri Mhagama ametekeleza maelekezo hayo leo Juni 17, 2025 kwa haraka ambapo amewajulia hali majeruhi hao pamoja na kutoa maelekezo kuwa wagonjwa hao (watano) watatibiwa kwa gharama za Serikali.
                        
                    
                    
                    
                        
                        
                                    
                                        
                                            🥹
                                        
                                    
                                        
                                            😂
                                        
                                    
                                    
                                        3