Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
June 18, 2025 at 04:23 AM
EIOS NYENZO MUHIMU KATIKA KUBAINI , KUFUATILIA NA UDHIBITI WA MAGONJWA-DKT. MMBAGA. Imeelezwa kuwa mfumo wa EIOS una mchango mkubwa katika Kutambua, kufuatili na udhibiti wa magonjwa hapa nchini. Hayo yamebainishwa leo tarehe 17, Juni, 2025 Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Epidemilogia na Udhibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Vida Makundi Mmbaga kwenye Mafunzo ya EPIDEMIC INTELLIGENCE FROM OPEN SOURCES- EIOS yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Dkt. Vida amesema mfumo huo una mchango mkubwa katika kuwajengea uwezo Wataalam wa ufuatiliaji na udhibiti wa Magonjwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ngazi ya Halmashauri na Mikoa. “Kuwepo kwa mfumo wa EIOS utasaidia katika kubaini Kwa haraka na kudhibiti wa magonjwa na matukio yanayoweza kuleta athari za afya katika jamii hivyo mifumo hii ni muhimu sana”amesema. Aidha, Dkt. Vida ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za tetesi za magonjwa kwa haraka Ili kuwezesha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa bila kusababisha athari kubwa , amesisitiza wananchi kupiga namba 199 kutuma tetesi za magonjwa Kwa wakati, huku akizungumzia namna jeshi kubwa la Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii lilivyo mstari wa mbele katika suala hilo” "Huwa tunafuatilia magonjwa ngazi ya jamii chini kabisa ngazi ya Kijiji na nyumba mojamoja , nitoe wito kwa jamii umuhimu wa kutoa taarifa kupitia 199 na jeshi letu la Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) limekuwa na mchango mkubwa sana “amesisitiza. Kwa upande wake Dkt. George Kauki mwakilishi kutoka WHO Tanzania amesema Mfumo wa EIOS hutumia teknolojia ya hali ya juu kama vile uchakataji na kuchambua mamilioni ya taarifa kila siku kutoka kote duniani na lengo kuu la mfumo huo ni kutambua viashiria vya mapema vya milipuko ya magonjwa na matukio mengine ya dharura ya kiafya kabla hayajaripotiwa na mamlaka rasmi. Naye Dkt. Joyce Nguna pamoja na Dkt. Sarah Fordah kutoka WHO Africa wamesema mfumo huo umesaidia nchi nyingi katika kugundua matukio ya kiafya mapema. Ikumbukwe kuwa “Epidemic Intelligence from Open Source-EIOS” ni Mfumo wa Kimataifa unaoongozwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) ambao unakusudia kuboresha uwezo wa kufuatilia na kukabiliana na magonjwa ya milipuko kwa kutumia taarifa zinazopatikana kutoka mifumo ya wazi zikiwemo vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, ikiwemo blog, tovuti za serikali na vyanzo vingine vya mtandao vinavyopatikana kwa umma. Mfumo wa EIOS hutumia teknoloji ambapo nchi ya Tanzania ilianza kutumia mfumo huu mwaka 2022 na umesaidia kufuatilia na kubaini magonjwa ya milipuko kwa sasa huku zaidi ya nchi 90 na mashirika 25 ya kimataifa na kikanda yanatumia mfumo huu na umesaidia kwa kiwango kikubwa kugundua magonjwa ya mlipuko mapema na hatua za udhibiti kuchukuliwa haraka.
Image from Wizara ya Afya Tanzania: EIOS NYENZO MUHIMU KATIKA KUBAINI , KUFUATILIA NA UDHIBITI WA MAGONJWA...

Comments