Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
June 18, 2025 at 03:58 PM
MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI WA RAIS SAMIA WAWAPIGA MSASA WATAALAM KITUO CHA AFYA UJIJI Na WAF, Kigoma Ujio wa Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Rais Samia uliofika katika kituo cha Afya Ujiji mkoani Kigoma umekuwa msaada kwa wenyeji wa kituo hicho kufuatia maelekezo ya namna ya kutumia chumba cha upasuaji kwa kufuata taratibu zote za kiupasuaji na namna ya kuzuia maambukizi eneo la kazi (IPC) kutoka kwa madaktari hao ambapo wamepata nafasi ya kuelekezwa , namna ya kutumia vifaa na miundombinu iliyopo. Bingwa Bobezi wa Upasuaji na Muuguzi Bobezi kutoka Wilaya ya Misenyi Mgana CDH Kagera Bw. Paschal Katunzi ameeleza kuwa pamoja na majukumu mengine ya kutibu wananchi wamekuwa na wakati mzuri wa kuelekezana na wenyeji wa maeneo waliopo katika kuwafundisha namna nzuri ya kiutendaji hasa katika eneo la huduma za upasuaji. "Pamoja na mambo mengine ya msingi tumewaelekeza namna bora ya kutumia vifaa na miundombinu yote kwa ujumla hasa katika maeneo ya kufanyia upasuaji ikiwa ni pamoja na IPC," amesema Bw. Katunzi. Kwa upande wake mwenyeji wa Kituo cha Afya cha Ujiji Bi. Magreth Lenard amesema ujio wa madaktari hao umekuwa msaada kwao kwani imewapa nafasi ya kupewa ujuzi na kuelekezwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na upande wa huduma za upasuaji . " Ujio huu ni mzuri sana kwetu kwani umetusaidia kujua mambo mengi yanayohusu masuala ya upasuaji. Namshukuru mama samia kwa kutuletea madaktari bingwa na bingwa bobezi," amesema Bi. Magreth.
Image from Wizara ya Afya Tanzania: MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI  WA RAIS SAMIA WAWAPIGA MSASA WATAAL...

Comments