
πππ ππππ‘ππ πππππ§ππππ₯π π¦ππ₯π©πππ, π§ππ‘πππ‘ππ
June 9, 2025 at 03:55 PM
Typhoid Fever ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na bakteria anayeitwa *Salmonella Typhi*. Bakteria huyu huingia mwilini kwa njia ya chakula au maji machafu yaliyo na kinyesi cha mtu aliyeambukizwa. Ugonjwa huu huathiri zaidi mfumo wa chakula, lakini pia unaweza kusambaa kwenye damu na sehemu nyingine za mwili.
Dalili za homa ya tumbo huanza taratibu na ni pamoja na homa ya juu inayoongezeka polepole, maumivu ya kichwa, uchovu, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kuharisha au kuvimbiwa, maumivu ya tumbo, na wakati mwingine vipele vidogo nyekundu kifuani. Bila matibabu, hali inaweza kuwa mbaya zaidi na kusababisha madhara kama kutoboka kwa utumbo au maambukizi ya damu(Sepsis)
Ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuepuka upungufu wa maji mwilini. Ili kujikinga, ni muhimu kunywa maji safi na salama, kula chakula kilichoandaliwa vizuri, kuosha mikono mara kwa mara, na kuhakikisha mazingira ni safi.
--------------------------------------
Article by: Dkt Fedrick, Telehealth Co
