
๐๐๐ ๐๐๐๐ก๐๐ ๐๐๐๐๐ง๐๐๐๐ฅ๐ ๐ฆ๐๐ฅ๐ฉ๐๐๐, ๐ง๐๐ก๐ญ๐๐ก๐๐
681 subscribers
About ๐๐๐ ๐๐๐๐ก๐๐ ๐๐๐๐๐ง๐๐๐๐ฅ๐ ๐ฆ๐๐ฅ๐ฉ๐๐๐, ๐ง๐๐ก๐ญ๐๐ก๐๐
๐ฏ๐บ๐๐บ ๐ง๐๐ฝ๐๐๐บ ๐๐บ ๐ฃ๐บ๐๐๐บ๐๐ ๐ช๐๐๐บ๐๐๐บ๐๐ ,๐ง๐๐ฝ๐๐๐บ ๐๐บ ๐บ๐ฟ๐๐บ ๐ญ๐๐๐๐ป๐บ๐๐ - ๐ง๐๐๐พ ๐ผ๐บ๐๐พ ๐๐พ๐๐๐๐ผ๐พ ,๐ฃ๐๐๐พ๐๐ ๐๐บ ๐ ๐ฟ๐๐บ ๐๐บ ๐๐๐บ๐๐ ๐๐บ ๐ ๐ฟ๐๐บ ๐๐๐บ ๐ด๐๐๐๐ ๐บ ๐๐บ ๐ฌ๐บ๐๐บ๐๐๐บ๐๐ ๐ฌ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐ง๐๐ฝ๐๐๐บ ๐น๐พ๐๐ ๐๐๐บ ๐ฉ๐บ๐๐๐. ๐ฏ๐บ๐๐๐๐บ ๐๐๐ป๐๐๐พ๐๐๐พ ๐ ๐ฟ๐๐บ ๐น๐พ๐๐ ๐๐๐บ ๐๐๐๐บ๐๐บ ๐ณ๐บ๐บ๐๐๐ฟ๐บ ๐ฌ๐๐๐๐๐ ๐๐บ ๐ฒ๐บ๐๐๐๐. ๐ฑ๐บ๐๐๐ป๐บ, ๐๐๐ ๐บ ๐ฒ๐๐๐ ๐ฉ๐๐๐บ๐๐บ๐๐ ๐ฌ๐๐บ๐๐บ ๐ฉ๐๐๐บ๐๐๐๐. ๐น๐๐๐๐บ๐๐๐บ ๐ฌ๐ฝ๐บ ๐๐ ๐๐๐บ๐๐๐๐บ ๐ฒ๐บ๐บ ๐ฌ๐ป๐๐ ๐ ๐ ๐๐๐ป๐๐๐ ๐ฌ๐๐บ๐๐บ ๐ฒ๐บ๐บ ๐ช๐๐๐ ๐ฉ๐๐๐๐. ๐ณ๐พ๐๐ป๐พ๐ ๐พ๐บ ๐ณ๐๐๐๐๐ ๐ธ๐พ๐๐ ๐ญ๐ฝ๐๐๐ https://linktr.ee/femclinic_hc ๐ค๐๐ฝ๐พ๐ ๐พ๐บ ๐๐๐๐บ๐๐๐ ๐๐บ๐๐บ ๐๐บ๐๐ ๐๐๐บ ๐ง๐๐ฝ๐๐๐บ ๐ก๐๐๐บ ๐๐บ ๐ ๐ฟ๐๐บ!โค
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

https://www.instagram.com/p/DKr9XbMtJUk/?igsh=NHhwZm56ZHQxbjRq

Habarini za Usiku ,Siku ya Kesho Dkt Fedrick Anapatikanaย kwaajili ya Huduma ya Onlineย Consultation .Kuanzia sasa unaweza kuweka Miadi na Daktari ๐10 June 2025 ๐คHuduma Hii ni Bure! ๐ทMatibabu ya Ugonjwa wa Typhoid ๐Weka Miadi https://t.co/xYNd016N2H โฐKuanzia Saa 4 Asbh Mpaka Saa 6 Mchana Dkt Fedrick, Telehealth Co Kwa kesi zote zinazosubiri ufuatiliaji tafadhali usisite kupiga Simu. 0747 290 565 , 0688 971 032 au Chati na Huduma kwa wateja WhatsApp https://wa.me/255747290559 #afyayauzazi#femclinic_hc#tunajalinakuthaminiafyayako#upati#drfedrickntashobo#clinician#sexualhealth&reproductivehealthcoach#vochadaychallenge


*Wapendwa, Habarini za Asubuhi! "Usiku ni Nusu ya kifo kuamka Salama ni Neema" Je, umeanza Siku yako kwa Sala ya kumshukuru Muumba?*

Kuvalisha uume kondomu ni hatua muhimu katika kujikinga na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa. Kondomu inapaswa kuvalishwa kabla ya uume kuingia kwenye uke, mdomo au sehemu nyingine yoyote ya kufanyia ngono. Hakikisha umechagua kondomu mpya, ambayo haijaisha muda wake wa matumizi na haijachanika. Fungua paketi kwa uangalifu bila kutumia meno au vitu vyenye ncha kali. Shika kondomu kwa upande wa ncha iliyo na kimoja kilichojaa hewa (teat) na bonyeza sehemu hiyo kwa vidole ili kutoa hewa na kuzuia kondomu kupasuka. Weka kondomu juu ya kichwa cha uume uliosimama, kisha ikunjue taratibu mpaka chini ya uume huku ukiendelea kushikilia ncha ya juu. Baada ya kumaliza tendo, ondoa kondomu kabla uume haujalegea kabisa, kwa kuishika kwenye shina la uume ili isije ikateleza. Funga kondomu na kuitupa kwenye pipa la taka, usiitumie tena. Kutumia kondomu kwa usahihi husaidia sana katika afya ya uzazi na kujikinga dhidi ya maambukizi. -------------------------------------- Article by: Dkt Fedrick, Telehealth Co

Mazoezi ya asubuhi huamsha mwili na kuupa nguvu ya kuanza siku vizuri. Husaidia kuimarisha mzunguko wa damu, kuongeza kiwango cha oksijeni mwilini, na kuchochea uzalishaji wa homoni zinazopunguza msongo wa mawazo kama endorphins. Mazoezi pia huongeza kasi ya kuchoma mafuta, kusaidia udhibiti wa uzito, na kuboresha usingizi wa usiku. Kwa kufanya mazoezi asubuhi, mwili huwa makini zaidi, kiwango cha nishati huongezeka, na mtu hujihisi vizuri kimwili na kiakili siku nzima. -------------------------------------- Dkt Fedrick, Telehealth Co #afyayauzazi#femclinic_hc#tunajalinakuthaminiafyayako#upati#drfedrickntashobo#clinician#sexualhealth&reproductivehealthcoach#vochadaychallenge


Kama hauwezi kudhibiti tamaa za Ngono Hautaweza kudhibiti Mambo Mengi kwenye maisha yako. Kichwa na Mdomo wa chini havijawahi kumuacha mtu salama. Take care, Good Night. See you Tomorrow ๐๏ธ -------------------------------------- Article by: Dkt Fedrick, Telehealth Co

Je, umewahi kukumbwa na tatizo la meno kuoza (Dental Caries)?

Dental caries hudhibitiwa kwa kuhakikisha usafi mzuri wa kinywa kila siku kwa kupiga mswaki angalau mara mbili kwa siku na kutumia dawa ya meno yenye fluoride. Ni muhimu pia kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi. Kutembelea daktari wa meno mara kwa mara kwa ukaguzi na kusafisha meno kitaalamu husaidia kugundua matatizo mapema. Matumizi ya vyakula vyenye madini ya kalsiamu na vitamini D pia kunasaidia kudumisha afya ya meno. -------------------------------------- Dkt Fedrick, Telehealth Co #afyayauzazi#femclinic_hc#tunajalinakuthaminiafyayako#upati#drfedrickntashobo#clinician#sexualhealth&reproductivehealthcoach#vochadaychallenge


Typhoid Fever ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na bakteria anayeitwa *Salmonella Typhi*. Bakteria huyu huingia mwilini kwa njia ya chakula au maji machafu yaliyo na kinyesi cha mtu aliyeambukizwa. Ugonjwa huu huathiri zaidi mfumo wa chakula, lakini pia unaweza kusambaa kwenye damu na sehemu nyingine za mwili. Dalili za homa ya tumbo huanza taratibu na ni pamoja na homa ya juu inayoongezeka polepole, maumivu ya kichwa, uchovu, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kuharisha au kuvimbiwa, maumivu ya tumbo, na wakati mwingine vipele vidogo nyekundu kifuani. Bila matibabu, hali inaweza kuwa mbaya zaidi na kusababisha madhara kama kutoboka kwa utumbo au maambukizi ya damu(Sepsis) Ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuepuka upungufu wa maji mwilini. Ili kujikinga, ni muhimu kunywa maji safi na salama, kula chakula kilichoandaliwa vizuri, kuosha mikono mara kwa mara, na kuhakikisha mazingira ni safi. -------------------------------------- Article by: Dkt Fedrick, Telehealth Co


Je, wewe hufanya mazoezi asubuhi?