
𝗙𝗘𝗠𝗖𝗟𝗜𝗡𝗜𝗖 𝗛𝗘𝗔𝗟𝗧𝗛𝗖𝗔𝗥𝗘 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗜𝗖𝗘, 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔
June 12, 2025 at 04:33 PM
Pelvic Inflammatory Disease ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke kama mji wa mimba, mirija ya uzazi na ovari. Mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria wanaosambaa kutoka kwenye uke hadi sehemu za juu, hasa kutokana na magonjwa ya ngono kama vile kisonono au chlamydia.
Mwanamke anaweza kutopata dalili mapema, lakini baada ya muda huweza kupata maumivu ya tumbo la chini, uchafu wa ukeni usio wa kawaida, maumivu wakati wa tendo la ndoa au kukojoa, na wakati mwingine homa.
Maambukizi haya yasipotibiwa mapema huweza kusababisha madhara makubwa kama vile utasa, mimba nje ya mji wa mimba au maumivu ya kudumu ya nyonga.
Kuzuia PID kunahitaji matumizi sahihi ya kondomu, kuepuka kuwa na wapenzi wengi na kupata matibabu ya haraka kwa magonjwa ya zinaa.
----------------------------------------------------
Dkt Fedrick, Telehealth Co
#afyayauzazi#femclinic_hc#tunajalinakuthaminiafyayako#upati#drfedrickntashobo#clinician#sexualhealth&reproductivehealthcoach#vochadaychallenge
