𝗙𝗘𝗠𝗖𝗟𝗜𝗡𝗜𝗖 𝗛𝗘𝗔𝗟𝗧𝗛𝗖𝗔𝗥𝗘 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗜𝗖𝗘, 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔
𝗙𝗘𝗠𝗖𝗟𝗜𝗡𝗜𝗖 𝗛𝗘𝗔𝗟𝗧𝗛𝗖𝗔𝗥𝗘 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗜𝗖𝗘, 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔
June 18, 2025 at 04:23 PM
*NAMNA YA KUDHIBITI MISULI KUKAZA NA KUKAKAMAA "MUSCLE CRAMP"* Kwanza Acha kufanya shughuli yoyote unayofanya na Anza kunyoosha Misuli iliyoathirika taratibu. Kuinyoosha husaidia kuirudisha misuli kwenye hali ya kawaida na kupunguza maumivu. Unaweza pia kufanya Masaji kwenye Misuli kwa kutumia Mikono Taratibu. Pili, Kanda Eneo la Msuli uliokaza kwa kutumia kitambaa cha Maji ya uvuguvugu. Unaweza tumia Maji ya Baridi au Barafu pia husaidia kupunguza maumivu kwa baadhi ya watu. Tatu, hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku kwa sababu upungufu wa maji mwilini ni mojawapo ya sababu kuu za misuli kukaza. Vilevile, kula vyakula vyenye Madini ya potasiamu, kalsiamu, na magnesiamu kama ndizi, Maziwa, na Mboga za majani husaidia kuzuia Muscle cramps. Iwapo misuli hukaza mara kwa mara bila sababu, Muone daktari kwani inaweza kuwa ishara ya tatizo la kiafya kama Matatizo ya neva, mzunguko wa damu au upungufu wa madini muhimu mwilini. ---------------------------------------------------- Dkt Fedrick, Telehealth Clinician #afyayauzazi#femclinic_hc#tunajalinakuthaminiafyayako#upati#drfedrickntashobo#clinician#sexualhealth&reproductivehealthcoach#vochadaychallenge
Image from 𝗙𝗘𝗠𝗖𝗟𝗜𝗡𝗜𝗖 𝗛𝗘𝗔𝗟𝗧𝗛𝗖𝗔𝗥𝗘 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗜𝗖𝗘, 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔: *NAMNA YA KUDHIBITI MISULI KUKAZA NA KUKAKAMAA "MUSCLE CRAMP"*  Kwanza...
👍 2

Comments