
𝗙𝗘𝗠𝗖𝗟𝗜𝗡𝗜𝗖 𝗛𝗘𝗔𝗟𝗧𝗛𝗖𝗔𝗥𝗘 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗜𝗖𝗘, 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔
June 20, 2025 at 06:33 AM
Mwanamke Ukiona Uchafu wa Njano unatoka ukeni inaweza kuwa ishara ya Maambukizi kwenye njia ya uzazi, hasa yanayosababishwa na bakteria kama vile Chlamydia au Gonorrhea, au Pia Trichomonas. Mara nyingi huambatana na harufu mbaya, kuwashwa, Maumivu wakati wa kukojoa au kujamiiana.
Mwanamke aliye katika hatari kubwa ni yule ambaye ana historia ya kubadili wapenzi mara kwa mara bila kinga, kutotumia kondomu, au aliye na mfumo wa kinga ulio dhaifu. Pia wanawake wajawazito wako katika hatari zaidi kwa sababu mabadiliko ya homoni huongeza uwezekano wa maambukizi.
Ni muhimu pia kuacha kujamiiana hadi Matibabu yatakapokamilika, kutumia kondomu mara kwa mara, na kuhakikisha mpenzi pia anapatiwa matibabu ili kuzuia maambukizi kurudi. Usafi wa sehemu za siri bila kutumia sabuni zenye kemikali pia husaidia kuzuia hali kama hizi.
----------------------------------------------------
Dkt Fedrick, Telehealth Clinician
#afyayauzazi#femclinic_hc#tunajalinakuthaminiafyayako#upati#drfedrickntashobo#clinician#sexualhealth&reproductivehealthcoach#vochadaychallenge
