Ashraf JK 💚💙
Ashraf JK 💚💙
June 11, 2025 at 07:17 PM
Kula chumvi nyingi pamoja na mazoezi machache ni njia ya haraka ya kupata shinikizo la damu. Fikiria mishipa yako ya damu kama mabomba ya maji. Unapokula chumvi nyingi, mwili wako unakusanya na kushikilia maji mengi zaidi. Hii inafanya mabomba (mishipa yako ya damu) kuwa na maji mengi na kuwa na msongamano kutokana na kiasi kikubwa cha damu kinachojaribu kupita. Fikiria umati wa watu unapojaribu kupita kwenye mlango mdogo; shinikizo/presha litakuwa kubwa! Hivyo ndivyo mwili wako unavyopata tabu unapokula chumvi nyingi. Sasa, kuhusu mazoezi: unaposhindwa kufanya mazoezi au unapofanya mara chache kana kwamba ni adhabu, misuli ya moyo inakuwa legevu na mabomba (mishipa ya damu) hayapanuki au kufanya kazi vizuri. Yanapoteza ufanisi wake na kuanza kukakamaa kama kipande cha raba/mpira kilichochoka. Kwa hivyo, ukiwa na maji mengi (kutokana na chumvi) na mabomba magumu (kutokana na kukosa mazoezi), moyo wako unapaswa kupiga kazi kwa bidii ili kusukuma damu mwilini kama kawaida. Kazi hii ya kupita kiasi inaweza kusababisha shinikizo la juu la damu. Ikiwa haitadhibitiwa vizuri, inaweza kusababisha kufeli kwa moyo, na kuleta shida mbaya zaidi za kiafya. PUNGUZA ULAJI WA CHUMVI, FANYA MAZOEZI. #afyatamu #kmt #ashrafjk

Comments